14 Aprili 2015

Mapigano yazuka upya Ukraine

Waasi walikuwa wamekubaliana kuondoa silaha nzito kama vifaru
Ukraine imesema kuwa imewapoteza maafisa wake 6 wa kijeshi katika kipindi cha saa 24 zilizopita kufuatia mashambulizi ya wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi.
Msemaji wa jeshi la Ukraine amesema kuwa kumekuwa na ufyatulianaja wa risasi usiku kucha.
Mapigano yameripotiwa kuendelea viungani mwa mji wa Donetsk.

Urusi kuiondolea Iran vikwazo vya silaha

 
Marekani imepinga hatua ya Urusi ya kuiondolea vikwazo vya silaha Iran, huku Urusi ikilenga kuipatia nchi hiyo mfumo wa kudhibiti makombora ujulikanao kama S-300.

Hatimaye Shamsa Ford Atoboa Kuwa Nay ndio “EndlessLove” Wake

Hatimaye Shamsa Ford Atoboa Kuwa Nay ndio “EndlessLove” Wake
Staa mrembo wa Bongo Movies Shamsa Ford ambae siku za hivi karibuni alikanusha waziwazi alipokuwa akihojiwa na vy mbo mablimbali vya habari juu ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi wa Staa Nay wa Mitego hatimaye jana kupitia ukurasa wake mtandaoni alibandikaa picha yake pamoja na ya Nay ankuandika maneno ya kimahada yaliyosomeka “Miss u so much my endlesslove.

Makundi ya waasi yanatumia ghasia za kingono kusambaza hofu

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema mwaka 2014 ulighubikwa na visa vya ubakaji, utumwa wa kingono na ndoa za lazima vilivyofanywa na wanamgambo wenye itikadi kali kuendeleza uasi wao.
Katika ripoti hiyo iliotolewa rasmi jana Jumatatu, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameelezea wasiwasi mkubwa alio nao kuhusu ghasia za kingono zinazofanywa na wanamgambo wa makundi yenye itikadi kali katika nchi za Iraq, Syria, Somalia, Nigeria Mali, Libya na Yemen.

Uwoya: Nimeshindwa Kuwa Rubani Sababu ya Filamu

Uwoya: Nimeshindwa Kuwa Rubani Sababu ya Filamu
Staa mrembo wa Bongo Movies, Irene Uwoya amesema kuwa filamu zimeharibu mipango yake ya miaka mingi ya kutaka kuwa mwongozaji wa ndege yaani Rubani.

Snura Aingizwa Mjini

Snura Aingizwa Mjini
Staa alieanzia Bongo Movie na kuingia kwenye Bongo Fleva Snura Mushi ‘Mama wa Majanga’ simu yake ya mkononi imetekwa na wajanja wa mjini kwa kuswap na simu anazopigiwa yeye kwenda kwa mtu mwingine ambaye hata hamjui wala hana mahusiano naye na hajui alitumia njia gani kuiteka hajui.

Watu 5 zaidi wauawa Afrika Kusini

 
 Wageni 5 zaidi wameuawa huko Durban
Watu watano zaidi wameuawa katika mashambulizi ya kibaguzi katika mji wa Durban nchini Africa Kusini.
Doria za maafisa wa polisi zimeimarishwa dhidi ya mashambulizi zaidi ya maduka yanayomilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa mengine ya afrika.

Ndege yatua mhudumu akilala ndani ya Shehena

Ndege ya abiria 170 yalazimika kutua mhudumu alipolaa ndani ya shehena ya mizigo
Ndege ya moja ya shirika la ndege la Alaska ililazimika kutua kwa dharura huko Seattle baada ya mhudumu wa ndege kugundulika alikuwa amesahaulika ndani ya sehemu ya kupakia mizigo ya ndege hiyo.
Rubani wa ndege hiyo alishtuliwa na mlio tofauti uliosikika ukitokea chini ya kiti chake na mara moja akaomba kutua kwa dharura.

Bibi,umri wa 65,ana mimba ya pacha wanne

Bi Raunigk aliyechangiwa mayai na mbegu za kiume anawatoto wengine 13 kutoka kwa baba watano tofauti.
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 65 kutoka Berlin Ujerumani ambaye ana watoto kumi na watatu ametangaza kuwa ni mja mzito na pacha wanne.

Hatimaye waliombaka Liz wahukumiwa Kenya

Hatimaye haki imetendeka baada ya watu watatu waliombaka msichana mdogo Liz kuhukumiwa kifungo cha mika 15 jela nchini Kenya
Mahakama moja mjini Busia, imewahukumu washukiwa watatu vifungo vya kati ya miaka saba na kumi na tano gerezani,baada ya kuwapata na hatia ya kumbaka na kumjeruhi msichana mmoja, aliyefahamika kama Liz.

Hiki Ndio Chazo cha Wema Kufunguka Kuwa Uwezo Hana Wakupata Mtoto

Hiki Ndio Chazo cha Wema Kufunguka Kuwa Uwezo Hana Wakupata Mtoto
Hivi juzi kati staa mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu aliandika kupitia ukursa wake mtandaoni akilelezea machungu aliyonayo kwa kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto lakini yote kamuachia Mungu hii ni kutokana na watu kumuandama sana mtandaoni kuhusu swala hilo. Sakata zima lilianzia hapa.

Irene Uwoya Aumizwa na Maneno ya Wema, Ampongeza Wema kwa Moyo Wakishujaa

Irene Uwoya  Aumizwa na Maneno ya Wema, Ampongeza Wema kwa Moyo Wakishujaa
“Minashindwa kuwaelewa watu ni kwanini mnapenda sana kutaka kutoa kibanz kwenye jicho la mtu wakat kipande chamti kiko kwenye jicho lako.....nimeumia sana na maneno ya wema,mtoto anapanga MUNGU sio binadamu .....Embu mwachen mtoto wa watu sasa awenaaamani kila siku mnamsema yeye mmnazan anachuma nin Ana moyo,afu kunawatu wanapenda sana kudandia mambo ........mmedandia weweee mme mtukana mtoto wawatu minaomba niwape namba ya MUNGU mumulize yeye kwanin na mumuache mtoto wa watu!sipendag kuingilia mambo ya watu lakin imezid sasaaaaa!!!!!sio vizuri jiweken nafas yake muone kama

Madonna ambusu Drake

Madonna ametibua mjadala baada ya kumbusu Drake jukwaani
Mwanamuziki mkongwe Madonna amejijengea sifa ya kutokua muoga katika maswala ya ngono wala ya kijamii.
Lakini alichokifanya mwishoni mwa juma liliwaacha wengi vinywa wazi .
Bibi huyo mwenye umri wa miaka 56 alishindwa kustahimili mvuto wa mwanamuziki wa kizazi kipya Drake alipokuwa akimwaga misstari mbele ya mashabiki wake katika onyesho
la California Coachella.

Gwajima: Kikwete wakemee polisi wanaoniandama

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuvikemea vyombo vya dola vinavyomfuatafuata vikihoji mambo binafsi na kwamba akishindwa kufanya hivyo itakuwa wazi kwamba yeye ndiye anawatuma.

Matukio 10 makuu baada ya mauaji Garissa


Polisi wakishika doria katika eneo la tukio Garissa

Familia za wanafunzi 142 kati ya watu 148 waliouawa katika shambulizi la kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa wameruhusiwa kuchukua miili ya wapendwa wao.
Familia zimeanza harakati za safari ya mwisho ya wapendwa wao baada ya serikali ya Kenya kuwaruhusu kuzichukua miili kutoka kwenye hifadhi ya maiti ya Chiromo jijini Nairobi.

13 Aprili 2015

Aaron Ramsey's early goal was enough for Arsenal to close the gap on leaders Chelsea to four points with a hard-earned victory at Turf Moor.

Aaron Ramsey Arsenal
  • Arsenal record eighth straight Premier League win
  • Burnley remain second from bottom of table
  • Aaron Ramsey nets ninth goal of the season
  • Disciplined away display from Wenger's side
Aaron Ramsey's early goal was enough for Arsenal to close the gap on leaders Chelsea to four points with a hard-earned victory at Turf Moor.
The Gunners have played two games more than Jose Mourinho's men, who play QPR on Sunday, so talk that they are now in a two-horse title race remains premature.

Picha: Wastara Anauliza, Hivi kwa Mfano….

Picha: Wastara Anauliza, Hivi kwa Mfano….Staa mrembo wa Bongo Movies, Wastara Juma amebandika picha hii mtandaoni akiwa na meneja wake Bond Bin Sinnan ni mtangazaji na pia ni muongozaji na muigizaji wa Filamu.
Kilichowafurahisha  wengi ni haya mameno Wastara alioyaandika kwenye picha huyo;
“Kwa mfano yaani no yaani nauliza hivi kwa mfano inakuwa ni aah basi nimeghairi tuendelee kuangalia mpaka usingizi utupitie uaminifu dhaifu hii ni TBTau Tabata Barakuda tuliambiwa cut ila cinema iliendelea”

Wakimbizi wa Somalia:UN yaijibu Kenya

Umoja wa mataifa unasema kuwa haujapokea amri rasmi kutoka kwa serikali ya Kenya ya kuutaka ufunge kambi ya wakimbizi ambayo ni makao kwa maelfu ya raia wa Somalia.
Siku ya jumamosi makamu wa rais wa Kenya William Ruto alisema kuwa amelipa shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa muda wa miezi mitatu ya kufunga kambi hiyo na kuwasafirisha wakimbizi hao kwenda nchini Somalia.
Amesema kuwa la sivyo Kenya itachukua jukumu hilo mikononi mwake.

Cesc Fabregas struck with three minutes to go as leaders Chelsea ground out a win against QPR at Loftus Roa

Joey Barton and Cesc Fabregas
  • Chelsea have one shot on target
  • Blues now seven points clear at top
  • QPR have 15 attempts on goal
  • Ivanovic hit by crowd missile
Cesc Fabregas struck with three minutes to go as leaders Chelsea ground out a win against QPR at Loftus Road.
The midfielder arrived late into the box and fired home from 16 yards after Eden Hazard and Oscar capitalised on a poor kick out by QPR's Rob Green.
Chelsea had not registered a single shot on target until then but did enough to extend their lead at the top of the Premier League to seven points.

How Chelsea can LOSE the Premier League title? Why Jose Mourinho's men aren't guaranteed winners


Chelsea's Portuguese manager Jose Mourinho looks on ahead of the English Premier League football match between Queens Park Rangers and Chelsea

All-conquering Chelsea have been looking down on all others since day one of this Premier League season.
The table-topping Blues hit the front early and have never looked back piling up wins and points on a relentless march to the title, a title their boss Jose Mourinho says his team more than deserve.
But is it all set in stone?

Justin Bieber brings Coachella Festival vibe down with foul-mouthed rant


Getty
Desert storm: Bieber squared up to a partygoer at Coachella Festival
It was never going to be a quiet weekend at Coachella once Justin Bieber rocked up.
The pop brat , sporting a ponytail, caused havoc backstage when he squared up to a partygoer, screaming: “You wanna f*** with me?”

Ester Awatoa Udenda Midume Hotelini

Ester Awatoa Udenda Midume HoteliniStaa mrembo wa Bongo Movies, Ester Kiama, juzikati aliwatoa udenda wanaume waliokuwa ndani ya Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi jijini Dar baada ya kutinga akiwa amevaa kivazi cha kihasara ile mbaya.
Ester aliingia hotelini hapo akiwa amevaa shati tu na kuacha wazi eneo la kuanzia mapajani, kitendo kilichowafanya wanaume wengi kuacha shughuli zao na kumkodolea macho.

Raia wa Sudan washiriki katika uchaguzi mkuu

Raia wa Sudan wameanza kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaobashiriwa kumrejesha madarakani Rasi Omar Al Bashir ambaye ameliongoza taifa hilo kwa miaka 25
Vyama vikuu vya upinzani nchini Sudan vinaususia uchaguzi huo unaoanza leo hadi Jumatano na hivyo inamaanisha rais wa sasa Bashir, mgombea wa chama tawala cha National Congress Party NPC anachuana na wagombea kumi na watano wa vyama vidogo vya kisiasa visivyojulikana au wagombea huru.

Abiria 18 wateketea ajali ya basi, lori

Morogoro. Watu 18 wameteketea kwa moto baada ya basi la Kampuni ya Nganga Express na lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la Iyovi, Milima ya Uduzungwa, Morogoro
Katika ajali hiyo iliyotokea jana saa mbili asubuhi, abiria 15 waliokuwa kwenye basi na wengine watatu wa lori waliteketea kwa moto huku wengine 10 wakijeruhiwa vibaya.

Pole Aunty Ezekiel kwa hili. Msamehe bure. Ni elimu tu.

Pole Aunty Ezekiel kwa hili. Msamehe bure. Ni elimu tu.Pole Aunty Ezekiel kwa hili. Msamehe bure. Ni elimu tu.
Kweli mitandao ya kijamii ina kazi. Ukiwa na moyo mwepesi mitandao hii inaweza kuwa sio wazo zuri sana kwako.

Butiku: Si dhambi kupigia Katiba kura ya hapana

Mbeya. Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema si dhambi kwa wananchi kupiga kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa.
Akizungumza juzi jioni kwenye mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na taasisi hiyo ambao ulifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku) jijini Mbeya, Butiku alisema kura ya Hapana au Ndiyo, zote zinatoa fursa sawa kwa wananchi kuamua kwa utashi wao.

Wema:azomewa licha ya Kujieleza

Muigizaji maarafu wa filamu nchini Tanzania,Wema Sepetu alizomewa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram
baada ya kuweka picha ya mlimbwende Hamisa Obetto akiwa mjamzito na kuandika maneno ya mshangao
”Jamani my mdogo umezaa.!wewe ni mwanamke sasa”.

11 Aprili 2015

Hawa Ndio Mastaa 10 Wakiume wa Bongo Movies Ambao Shamsa Anawakubali

Hawa Ndio Mastaa 10 Wakiume wa Bongo Movies  Ambao Shamsa AnawakubaliStaa mrembo wa Bongo Movies, Shamsa Ford ambae ni Binamu Wa Nay Wa Mitego amewataja hawa kua ndio wakali wake.
“Mambo vipi Tanzania? Leo ningependa kuwatajia wanaume 10 ambao huwa napenda sana uigizaji wao, haimanishi kwamba wao ndo the best kuliko wengine but napenda tu sanaa yao. (1) Single Mtambalike ‘Richie’ (2) Marehemu Adamu Kuambiana (3) Marehemu Kanumba

KAULI YA WEMA YALIZA WENGI. Aweka wazi kuwa hawezi kupata mtoto.


KAULI YA WEMA YALIZA WENGI. Aweka wazi kuwa hawezi kupata mtoto.Kumbukeni na mimi pia ni binaadam... Nina moyo kama nyie... Au mnadhani napenda kuona wenzangu wana watoto au wana ujauzito alafu mimi sina hata wa kusingiziwa... Mnaona nafurahia sio.... Hivi mna nini jamani... Yaani mtu unaweza weka post kwa nia nzuri then people just come from nowea wanaanza kukuandikia maneno ya kukuumiza kabisa nafsi hadi mtu unakaa unajiuliza umemkosea nini mwenyezi Mungu...

Diamond Atoa Kiapo, Wema Ajibu Mapigo

Diamond Atoa Kiapo, Wema  Ajibu MapigoStaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amefungukia msimamo wake juu ya mwandani wake wa zamani, Wema Sepetu ‘Madam’ kwa kusema kuwa kamwe hawezi kumrudia tena.

09 Aprili 2015

Eti Maya, Johari Wana Gundu!

Eti Maya, Johari Wana Gundu!Staa wa Bongo Movies, Mayasa Mrisho ‘Maya’, amefunguka kuwa anahisi yeye na mwigizaji mwenzake ambaye ni mkongwe, Blandina Chagula ‘Johari’ wana gundu kwani wasanii wenzao wengi wana watoto na wengine ni wajawazito lakini wao wapowapo tu.

MGOMO WA MAGARI UMEANZA


- Jijini Dar, wananchi wametembea kwa miguu na wengine kupanda malori ya mchanga!

Mgomo wa Madereva umeripotiwa kuanza asubuhi ya Leo sehemu mbalimbali Nchini

MAMBO YA SIASA

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ameshiriki kikamilifu kubomoa misingi ya taifa hili. Ni kutokana na kutaka kuwapo Mahakama ya Kadhi nchini. Anaandika Eberi M. Manya … (endelea).

ABIRIA WAFANYA UHARIBIFU TRENI MPYA


Siku chache baada ya kuzinduliwa kwa treni mpya ya abiria (Deluxe), abiria wa awali kutumia usafiri huo kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, wamekosa ustaarabu na kufanya uharibifu katika baadhi ya mabehewa.

Mgomo wa madereva nchi nzima wanukia

Madereva wa vyombo mbalimbali vya moto, wanakusudia kushiriki mgomo wa nchi nzima Ijumaa wiki hii, kuishinikiza serikali kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ajira za uhakika pamoja na agizo la kutaka kwenda kusoma.
Wakizungumza kupitia Katibu wa Muungano wa vyama vya madereva Bw. Rashid Saleh, Madereva hao wameiambia East Africa Radio kuwa suala la kurudia kusoma kila wanapohuisha leseni zao ni aina nyingine ya unyanyasaji kwa maelfu ya madereva nchini, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana mfumo mzuri wa ajira licha ya kutupiwa lawama kibao kuwa wao ndio chanzo cha ongezeko la ajali.

Yoshinori Muto: Chelsea make bid for Japanese striker

FC Tokyo striker Yoshinori Muto Japanese news agency Kyodo News says the FC Tokyo player is yet to decide whether to move to Stamford Bridge in the summer.
The 22-year-old, capped 11 times, has scored three times in four games at the start of the new J-League season.
Muto, who scored 13 times last season and was named in the league's select XI, played for Japan during their run to the quarter-finals of the Asian Cup.
He retained his place in the squad selected by new coach Vahid Halilhodzic for his first matches in charge last month.
Muto graduated in economics from Keio University two weeks ago.
In February, Premier League leaders Chelsea announced a new shirt sponsorship deal with a Japanese tyre manufacturer worth a reported £40m a year.

Ajali: Mabasi ya Ngorika na RATCO yamegongana uso kwa uso na kusababisha vifo

Name:  IMG-20150409-WA0008.jpg
Views: 0
Size:  119.7 KB
Watu 10 wamekufa katika ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata katika Kijiji cha Mbweni Wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya jana.

Rose Ndauka, Shetta Wadaiwa Kulala Chumba Kimoja

Rose Ndauka, Shetta Wadaiwa Kulala Chumba KimojaChanzo makini kinachofahamu kwa undani kinachoendelea baina ya mastaa hao wawili, kimelidokeza gazeti la Amani kuwa tukio hilo lilijiri wakati wakielekea katika shughuli za mazishi ya muasisi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge aliyezikwa kijijini kwao Mkuyuni mkoani humo, ambako watu wengi maarufu walihudhuria.

Jaji na wakili wapigwa risasi Italy

 
Jaji mmoja na wakili ni miongoni mwa watu waliouawa baada ya mshukiwa mmoja kuwafyatulia risasi ndani ya mahakama moja mjini Milan nchini Italia.

Aunt Ezekiel Alia Mimba Kumkosesha 'Madili'

Aunt Ezekiel Alia Mimba Kumkosesha 'Madili'
Staa mrembo wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel, amesema kwamba anatamani kujifungua, kwani amechoshwa na mimba yake, kwa sababu imemfanya ashindwe kupata kazi ya kucheza filamu nyingine.

Somalia puts bounty on al-Shabab leaders

Al-Shabab militantsSomalia's government has placed a bounty on the top 11 leaders of the militant Islamist al-Shabab group.
Top of the list is its chief Ahmed Diriye with $250,000 (£169,000) offered for information leading to his capture.

Kajala Atamani Kumlipa Wema Mil.13 Zake

Kajala Atamani Kumlipa Wema Mil.13 ZakeStaa  mrembo  wa Bongo Movies, Kajala Masanja  kwa mara ya kwanza  ameibuka  na kutoa ya moyoni kuwa anatamani kulipa shilingi milioni 13 alizolipiwa na staa mwenzake  Wema Sepetu kama faini ili asiende jela miaka saba.
Akizungumza na gazeti la Amani, Kajala  alisema  kuwa huwa anaumia sana kila anapokumbuka kuwa alipewa kiasi hicho chapesa ingawa uwezo wa kulipa anao.

Mourinho:Taji la mchezaji bora lifutwe

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho anaamini kwamba taji la mchezaji bora duniani Ballon d'Or linafaa kuondolewa.
Mourinho anasema kuwa lengo la soka linabadilika kutoka timu za soka hadi kwa wachezaji binafsi.
''Tuanaangazia mchezo wa mchezaji mmoja, pasi alizotoa na amekimbia kilomita ngapi uwanjani.Pengine ulikimbia kilomita 11 na mimi nilikimbia kilomita tisa,lakini kilomita zangu zilikuwa muhimu kushinda zako'',alisema Mourinho.
Amesema kuwa Chelsea boss Jose Mourinho believes the Ballon d'Or should be scrapped.
Je, unadhani FIFA inafaa kulifutilia mbali taji la mchezaji bora duniani.Ingia katika mtandao wetu wa facebook katika bbcswahili uweke maoni yako.

Haya Ndio Malalamiko ya Mama Kanumba kwa Lulu

Haya Ndio Malalamiko ya Mama Kanumba kwa LuluStaa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mama wa aliyekuwa nyota wa fani hiyo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa wamefikia pabaya baada ya mama huyo kumshushia Lulu maneno  makali na ya shutuma.

Tanzania imeshindwa kuzifanya nyayo za binadamu wa kale kivutio cha utalii

Ukisoma vitabu vya historia utaona kuwa nyayo za mtu wa zamani aliyeanza kutembea kwa miguu miwili zilipatikana katika Kijiji cha Endeluni, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Kijiji hiki kipo kilometa 34 kutoka Makao Makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na eneo halisi lenye alama hizo za historia ya binadamu linajulikana kama Laetoli.

Nchi inaibiwa kwa kutumia mfumo wa kukusanya kodi

Sakata la wafanyabiashara kufunga maduka kwa siku kadhaa katika baadhi ya miji nchini wakipinga matumizi ya Mashine za Risiti za Kieletroniki (EFD) limeelezwa kukumbwa na vikwazo kutoka kwa baadhi ya vigogo kunufaika na mashine hizo.

Mambo sita yaliyomshinda Rais Kikwete


Rais Jakaya Kikwete alitoa ahadi lukuki kwa makundi mbalimbali ya jamii katika kipindi cha miaka 10 ya utawala wake kupitia kaulimbiu yake ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, lakini anaondoka madarakani mwaka huu akiwa ameshindwa kutekeleza ahadi nyingi  na zaidi ameacha manung’uniko na mgawanyiko.
Mwaka 2005, alipoingia madarakani aliahidi kuondoa uhasama wa kisiasa kati ya visiwa vya Unguja na Pemba, kuondoa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, kuwapatia wanahabari Sheria ya Habari, kupambana na ufisadi; na mwaka 2010 aliahidi kuwapa Waislamu Mahakama ya Kadhi na wananchi Katiba Mpya.

Bei za vyakula zapaa, mfumuko wa bei mwezi Machi wafikia asilimia 4.2

Dar es Salaam. Upungufu  wa chakula kwa baadhi ya mikoa nchini umeendelea kusababisha ongezeko la mfumuko wa bei wa Taifa kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 4.2 ndani ya mwezi mmoja.
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraimu Kwesigabo, aliwaambia waandishi wa habari leo kuwa, kutokana na upungufu huo bei za bidhaa za vyakula zimeongezeka.

BAKORA SITA ZA UKAWA KWA CCM

Dar es Salaam. Uhakika wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutamba katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba utategemea umahiri wake katika kukabiliana na vikwazo sita vinaonekana kuwa mwiba kwake ambavyo upinzani kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unatarajiwa kuvitumia kama mtaji wake katika kampeni.

Lowassa: Natazamwa na CCM kila kona

Dar es Salaam. Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amesema anashindwa kujitokeza kuzungumzia au kufanya mambo yanayohusiana na urais kwa kuwa Kamati ya Maadili ya CCM inamfuatilia kwa karibu.
Alisema hayo jana alipoulizwa kuhusu kauli ya Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita akiwa Marekani ambako alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10.

08 Aprili 2015

Mchezaji wa EPL anaswa kwa wizi London

Mchezaji wa zamani wa ligi kuu ya premia ya Uingereza Andrea Dossena amekamatwa kwa kuiba bidhaa dukani.
Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Leyton Orient anadaiwa kuwa aliiba katika duka moja la kifahari la Harrods lililoko jijini London.
Awali Andrea aliwahi ichezea timu ya Liverpool.
Andrea alikamatwa na maafisa wa polisi kutoka kituo cha Brompton Road, Knightsbridge.
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728