09 Aprili 2015
Aunt Ezekiel Alia Mimba Kumkosesha 'Madili'
Staa mrembo wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel, amesema kwamba anatamani kujifungua, kwani amechoshwa na mimba yake, kwa sababu imemfanya ashindwe kupata kazi ya kucheza filamu nyingine.
Akizungumza na gazeti la Mtanzania jana, msanii huyo alisema kuwa mialiko ya kucheza filamu imekata na sasa haingizi kipato chochote, badala yake pesa inatoka, hali ambayo inamfanya atamani ajifungue ili aondokane na adha hiyo.
“Siyo siri nimechoshwa na hii mimba, natamani hata leo nijifungue, kwani sipati tena tenda za kwenda kuigiza ambazo huwa zinaniingizia pesa ya kujikimu na sijui lini nitajifungua,” alisema msanii huyo.
Aunt Ezekiel, ambaye aliigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu ya Chozi la Mwanjaa, alisema kwamba anatambua ujauzito ni baraka na kuna watu wanatamani kupata mimba na hawapati, lakini wakati mwingine ni kama adhabu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni