Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mama wa aliyekuwa
nyota wa fani hiyo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa wamefikia pabaya baada
ya mama huyo kumshushia Lulu maneno makali na ya shutuma.
Kwa mujibu wa Gazeti la Amani, inadaiwa kuwa mama Kanumba
amemlalamikia Lulu kwamba, amemtupa na kumtenga tofauti na zamani ambapo
uhusiano wao ulikuwa kama wa mama na binti yake.
Akizungumzia swala hilo kwa njia ya simu mama Kanumba alilieleza gazeti hilo kinaga ubaga
“Lulu si Lulu yule jamani. Lulu sasa hivi amebadilika. Awali
aliniambia hatanitupa, lakini sivyo. Lulu siku hizi haji kunisalimia
wala hanipigii simu.”
“Imefika mahali nawaza kwamba, huenda alipenda Kanumba aondoke ili yeye
apate mafanikio makubwa aliyonayo sasa. Lulu amenitenga, amenitenga,
amenitenga!” , Mama Kanumba alisema.
Juzi, Jumanne, ambayo ilikuwa siku ya kuadhimisha mwaka wa tatu tangu
kifo cha staa huyo, mama huyo alishiriki kwa kwenda kwenye Makaburi ya
Kinondoni jijini Dar kwa lengo la kusafisha kaburi la mtoto wake. Baada
ya zoezi la kusafisha kaburi kumalizika, mama Kanumba aliongea na Amani
na kuyasema haya:
“Nasikitika sana namna ambavyo Lulu amekuwa tofauti na maneno yake ya
zamani kwamba atakuwa sambamba na mimi katika kuadhimisha kumbukumbu ya
Kanumba. Lakini leo kama hivi, hajatokea.
“Pia nasikitishwa na kitendo cha kufanya bethidei ya mdogo wake jana
(Jumatatu usiku) kule Posta wakati anajua ndiyo usiku ambao Kanumba
alifariki dunia.
“Mbaya zaidi, akiulizwa na watu kwa nini sasa hivi hayupo sambamba na
mimi kama zamani, anajibu majibu ambayo hayaeleweki. Kumbe maneno yake
ya zamani kwamba atakuwa sambamba na mimi yalikuwa ya usaliti.
“Kwa hiyo na mimi sasa nimeamua kubaki peke yangu kama nilivyo,
nitaendelea kumuenzi Kanumba mwanangu kwa sababu mimi ndiyo mama yake
kwa hiyo nalia peke yangu.”
Katika mazungumzo yake, mama Kanumba alikwenda mbali zaidi kwa
kusema: “Kuna siku aliahidi kwamba atajengea picha ya Kanumba ikiwa
ndani ya kioo na kuiweka juu ya kaburi, hajafanya hivyo. Nitafanya
mwenyewe.“Labda amepuuza kwa vile anajiona anazidi kukua kisanii, ni
supastaa ndiyo maana anatoa ahadi za uongo.”
Lulu alipotafutwa juzi na gazeti hilo kuzungumzia malalamiko ya mama
mkwe wake huyo, hakupatikana lakini wiki iliyopita alizungumza na
paparazi wetu kuhusu mtazamo wa maisha yake kwa jumla ambapo
alisema:“Mimi kwa sasa hivi nina mtazamo mwingine kabisa kuhusu maisha.
Kwanza sidhani kama nitamwaga machozi tena kuhusu Kanumba maana nimelia
sanasana.“Mtu ambaye naweza kumlilia ni mama yangu (Lucresia Karugila)
na mdogo wangu. Lakini si mtu mwingine. Kwa sasa naangalia zaidi familia
yangu.”
09 Aprili 2015
Haya Ndio Malalamiko ya Mama Kanumba kwa Lulu
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni