26 Mei 2015

Nchi za EAC kukutana mwishoni mwa Juma

Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika Mashariki na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Wizara ya Mambo ya nje Tanzania imetoa taarifa juu ya kuwepo kwa mkutano wa Viongozi wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili ili
kuangalia kwa mara nyingine tena hali ya amani nchini Burundi.
Jaribio la mapinduzi la kijeshi lililofanyika Mei 13 wakati Rais Pierre Nkurunziza akiwa nje ya nchi katika mkutano wa maraisi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulifeli,na Rais kulazimika kurejea Burundi.
Mkutano huu unaotarajiwa kufanyika karibuni haujaweka wazi kama Raisi huyo wa Burundi atakuwepo ila umeweka bayana kuwa Burundi itawakilishwa vyema.
Upinzani nao nchini humo umegoma kufanya mazungumzo baada ya mmoja wa viongozi wake kuuwawa siku ya Jumamosi.
Machafuko ya sasa yamesababisha zaidi ya Raia 100,000 wa Burundi kukimbilia nchi za jirani Rwanda, Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728