16 Mei 2015

Wafanya mzaha kuhusu alipo Nkurunziza

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza
Wakati raia wa Burundi wakiwa wanasubiri Rais wao Pierre Nkurunziza kulihutubia taifa baada ya kurejea nchini kwake kufuatia jaribio la Mapinduzi lililoshindwa,baadhi ya
watu kutoka maeneo mbalimbali barani Afrika wametupa picha nyingi za mizaha zinazoonyesha wanamtafuta Rais huyo katika mazingira yasiyo ya kawaida kama vile ndani ya majokofu na chini ya viti.
Rais Pierre Nkurunziza amedai kuwa amesharejea nchini mwake baada ya kukwama nchini Tanzania kutokana na tishio la usalama kufuatia jaribio la mapinduzi.
Viongozi watatu walioendesha jaribio hilo tayari wameshakamatwa huku Umoja wa Mataifa ukikadiria kuwa zaidi ya watu 100,000 wameikimbia nchi hiyo kwa hofu.
Watumiaji wa mtandao wa Twitter kutoka pande mbali mbali barani Afrika usiku kucha wamechangia mara 2000 katika hashtag, iliyosema "Where is Nkurunziza"
Nkurunziza
Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa tweeter kutoka mji wa Bujumbura, Kris Nsabiyumva, aliwasilisha ujumbe mara kadhaa akiomba msaada kutoka kwa msanii maarufu wa vikaragosi kutoka Marekani Dora kusaidia kumtafuta Rais Nkurunziza huku akiendelea kumtafuta pia chini ya kochi lake.
Naye mmiliki wa blogu ijulikanayo kama Mr Burundi kwa siri alionekana akiyaambia maua yake kuwa,Shangazi yake kaniambia kuwa Nkurunziza ameonekana eneo la Ngozi na kwamba amemuona kwa macho yake, na kwamba wamempata.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728