Rais wa Nigeria anayeondoka Goodluck Jonathan, ameonya dhidi ya kuwatesa mawaziri walohudumu katika utawala wake.
Jonathan ameonya kuwa mawaziri waliohudumu katika utawala wake wamo katika hatari ya kuteswa pindi mrithi wake Muhammadu Buhari atakapochukua wadhfa.
Matamshi hayo yanakisiwa kuashiria kuwa labda Jonathan anahofu kuwa uchunguzi wa ubadhirifu wa mali ya uma na ufisadi huenda ukawalenga mawaziri wake.
Rais Jonathan ndiye kiongozi wa kwanza wa Nigeria kuondolewa afisini baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu mwezi Machi.
Jonathan alishindwa na kiongozi wa upinzani jenerali mstaafu Muhammadu Buhari.
Majuzi Jonathan alikiri kutengwa na watu aliodhani kuwa ni wandani wake baada yake kushindwa .
Jenerali Muhammadu Buhari anatarajiwa kuapishwa rasmi na kuchukua mamlaka tarehe 29 Mwezi huu.
Inaaminika kuwa wandani wa karibu wa Jonathan hawakufurahia alipokubali kushindwa katika uchaguzi uliopita.
''tunajua vyema kuwa uamuzi wako wa kibinafsi unaweza kuwaudhi watu unaowadhani kuwa ni marafiki wako''
Najua vyema pia kuwa mawaziri wangu huenda wakahujumiwa na nilazma wawe tayari kwa mateso hayo yote ''alisema Jonathan katika hotuba yake kanisani.
Katika kampeini jenerali Buhari aliahidi kukabiliana na zimwi la ufisadi ambalo alidai linaisakama uchumi wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi Afrika.
Rais Jonathan alitawazwa kuwa rais mwaka 2010 baada ya kuaga dunia kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Umaru Musa Yar'Adua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni