Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance kimemteua mwafrika kwa kwanza kukiongoza .
Wajumbe katika kongamano kwenye mji wa Port Elizabeth walimteua Musi Maimane kukiongoza chama hicho.
Bwana Maimane mwenye umri wa miaka 34 tayari anakiongoza chama hicho bungeni.
Waandishi wanadai kuwa Chama hicho cha Democratic Alliance kimekuwa kikionekana kama kinchowawakilisha watu weusi lakini sasa kinajaribu kujibadilisha ili kupata kuungwa mkono katika maeneo yote.
Hatahivyo wakosoaji wanasema kuwa Maimane hana ujuzi wa kukiongoza chama hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni