21 Mei 2015

Al Shabaab wavamia msikiti Garissa

Al Shaabab waliuteka msikiti mmoja katika kaunti ya Garissa kwa muda na kuonya wenyeji dhidi ya kuisaidia serikali ya Kenya na ujasusi
Viongozi Kaskazini mwa Kenya wamesema kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi kutoka Somalia la Al Shaabab waliuvamia msikiti
mmoja katika kaunti ya Garissa kwa masaa kadhaa.
Wapiganaji hao waliwahutubia waumini waliokuwa msikitini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea mwituni.
Waliikosoa serikali ya Kenya na kuonya waumini dhidi ya kuwa majasusi wa serikali ya Kenya.
Mwezi uliopita Al Shaabab walivamia chuo kikuu cha Garissa na kuwaua watu 150 wengi wao wanafunzi.
Kundi hilo kutoka Somalia linaaminika kuwa na wafuasi nchini Kenya ambapo limetekeleza mashambulizi kadha katika jitihada ya kuilazimisha serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom ambao wanaisaidia serikali dhaifu ya Somalia kupigana na waasi wa Al Shabaab.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom
Msikiti huo upo takriban kilomita 40km kutoka mji wa Garissa kulikotokea shambulizi la chuo kikuu mwezi uliopita.
Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji hao walikuwa wameandamana na wapiganaji takriban 40 waliojihami tayari kwa vita.
Mwandishi wa BBC Abdullahi Abdi aliyeko mjini Nairobi anasema kuwa serikali ya Kenya imeanza kujenga ua ilikuzuia mashambulizi kama hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728