Bayern Munich imesema kuwa itang'ang'ana hadi dakika ya mwisho kubadilsha matokeo ya 3-0 dhidi ya Barcelona wakati timu hizo zitakapokutana leo.
Mabingwa hao wa Ujreumani walishindwa 3-1 dhidi ya Porto katika mechi ya robo fainali kabla ya kubadilisha matokeo hayo na kuwa 6-1.
Mkufunzi wa Bayern Pep Guardiola ambaye alikuwa akiifunza Barcelona amesema:''Njia ya pekee itakayotuhakikishia tumeingia fainali ni kucheza zaidi ya Barcelona na kufanya vile tulivyofanya dhidi ya Porto.''Mpango wetu ni kujaribu hadi mwisho''.
Mabingwa hao wa Ujreumani wanacheza bila Franck Ribery na Arjen Robben.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni