Filamu kali na ya kusisimua ya Anko Kiepe imeingia sokono leo tarehe 11 na
imesambazwa nchi nzima hivi karibuni akiongelea filamu hiyo mungozaji na mtunzi wa filamu hiyo Phelimon Lutwaza anasema kuwa ni kazi ya kipekee na anaonyesha uwezo wake kwa kufanya maajabu makubwa.
“Anko Kiepe inakuja kufanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Bongo Movie nimefanya mambo makubwa sana katika sinema hii kiuigizaji shutingi na wasanii wameitendea haki sinema hii, pia nimeiongoza mwenyewe,”anasema Lutwaza.
Filamu ya Anko Kiepe imewashirikisha wasanii nyota kama Patcho Mwambo, Phelimon Lutwaza, Yobnesh Yusuf na wasanii wengine wanaofanya vinzuri katika tasnia ya filamu na filamu hiyo inasambazwa na kampuni ya B.M.O nunua nakala halisi kukuza vipaji vya wasanii wa Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni