Maelfu ya raia wa Burundi wakisubiri kupokewa katika mji wa Kagunga nchini Tanzania. Raia wamelazimika kuikimbia nchi yao kufuatia ghasia zinazosababishwa na maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania awamu ya tatu uongozini. Hii leo milio ya risasi imesikika katika vitongoji vya mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, huku vijana wanaoandamana kumpinga Rais Nkurunziza wakiwarushia mawe polisi wanaojaribu kudhibiti hali. Nao viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana kesho jijini Dar es Salaam, Tanzania, kuzungumzia hali inayozidi kutokota nchini Burundi. Je, unadhani mkutano huu utaleta suluhu yoyote katika
mgogoro wa Burundi? Tupe maoni yako.
12 Mei 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni