Balozi wa Libya kwenye Umoja wa Mataifa anasema kuwa nchi yake itapinga jaribio la muungano wa ulaya kutaka kuundwa kwa jeshi litakalokabiliana na walanguzi wa binadamu katika bahari ya mediterrania .
Ibrahim Dabbashi aliambia BBC kuwa hakukua na majadilianona Libya kuhusu suala hilo.
Umoja wa Ulaya ulikuwa umependekeza kupitishwa kwa azimio litakaloruhusu kuundwa kwa jeshi litakalokabiliana na walanguzi wa watu.
Balozi wa Umoja wa Ulaya katika Umoja wa Mataifa ,Federica Mogherini, anatarajiwa kuhutubia baraza la usalama la umoja wa mataifa baadaye leo.
Jana Jumapili shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilisema kuwa wahamiaji wanahatarisha maisha yao kufika bara ulaya kwa sababu wanakabaliwa na hatari ya kutekwa , mateso na ubakaji nchini Libya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni