12 Mei 2015

Mama aibiwa mtoto kliniki Mkoani Morogoro

Name:  mtoto.png
Views: 0
Size:  312.3 KB

Martha Masawe akilia kwa uchungu baada ya kuibiwa mwanae.
Inauma sana! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Martha Masawe (20), mkazi wa Kilakala mkoani hapa, ameibiwa mtoto mchanga mwenye umri wa siku 34 akiwa katika Hospitali ya
Nunge, Ijumaa Wikienda lina ‘full’ stori.

Tukio lililofanywa kimafia lilijiri Ijumaa iliyopita saa 7:00 mchana wakati Martha akiwa kwenye foleni.

Akihojiwa na Ijumaa Wikienda huku akiangua kilio hospitalini hapo Martha alisema:

“Usiku wa kuamkia leo (Ijumaa) mwanagu alikohoa sana, asubuhi baba yake aliniambia nimlete hospitali kucheki kifua.

“Nikiwa kwenye foleni alikuja mama mmoja, akaomba amshike mwanangu huku akisema ni mzuri.

“Baadaye aliniuliza ana tatizo gani? Nikamwambia anaumwa kifua, akanishauri twende dukani tukamnunulie sweta.

“Tulikwenda maduka ya Kikundi tukanunua sweta na nguo nyingine kisha kila mtu akapanda bodaboda yake tukaanza safari ya kurudi hospitali.

“Chaajabu nafika hapa hospitali nimekaa zaidi ya nusu saa yule mama hajatokea. Nikawasimulia manesi wakadai tayari nimeibiwa mtoto.”

Baadaye mama huyo alipata msaada wa askari wa doria, afande Mwajabu aliyeongozana naye kwenda kituo cha polisi kufungua mashtaka na namna ya kumuelewesha mumewe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728