Klabu ya Yanga itamkosa mshambuliaji wake, Mrisho Ngassa katika msimu wa ligi kuu na mechi za
kimataifa mwakani kufuatia habari za mchezaji huyo kusaini kuchezea klabu ya Free State ya Afrika ya Kusini kwa miaka mitatu.
Klabu hiyo ilimtaka mchezaji huyo mwaka jana kwa dau la dola 80,000 lakini klabu yake ilitaka ilipwe dola 150,000. Ngasa alionesha ishara ya kuiaga klabu Yanga katika sherehe za kukabidhiwa kombe la ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuvua jezi zake na fulana yake ya ndani ikisomeka “ I will always love Yanga, Thanx, Bye” akimaanisha kuwa ataipenda Yanga siku zote katika maisha yake, asante, kwaheri Yanga.
Ngasa aliwahi kufanya majaribio katika klabu kadhaa ikiwemi Timu ya West Ham ya Uingereza mwaka 2009 ikiwa chini ya kocha Zola lakini hakufanikiwa. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Ngasa atajiunga rasmi na timu hiyo mwezi July akiwa mchezaji huru. Ngasa ameisaidia Yanga kutwaa ubingwa na amekuwa mfungaji na kiungo muhimu katika kusababisha magoli
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni