16 Julai 2015

Jeshi la Japan sasa kupigana nje


Shinzo Abe bungeni
Bunge la uwakilishi la Japan, limeidhinisha kifungu cha sheria ya usalama yenye utata inayoleta mabadiliko inayoliruhusu jeshi la
nchi hiyo kupigana katika mataifa ya kigeni tangu wakati wa kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.
Mabadiliko hayo ambayo yalipigiwa upatu na waziri mkuu Shinzo Abe, ambaye anasema kuwa itairuhusu Japan kukabiliana na vitisho hasa kutoka China.
null
Jeshi la Japan
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni Hua Chunying, ameitaka Japan isalie katika njia ya maendeleo ya amani na kusaidia majirani zake.
Mabadiliko hayo yalianzishwa na waziri mkuu, Shinzo Abe, anayeamini kuwa ni muhimu kukabiliana na changamoto mpya inayoikabili Japan, hasa kutoka China.
Lakini wapinzani wanaamini kuwa marekebisho hayo, yanakiuka katiba ya Japan iliyobuniwa baada ya vita na inaweza kuyumbisha usalama wa taifa hilo, katika mzozo unaoongozwa na Marekani.
null
Raia wa Japan wapinga sheria ya kuliruhusu taifa hilo kushiriki katika vita vya kimataifa
Baada ya hotuba kadhaa wakati wa mjadala huo bungeni, vyama vya upinzani vilikataa kuhudhuria shughuli za upigaji kura.
Kumeshuhudiwa upinzani mkali dhidi ya mabadiliko hayo, hali iliyosababisha kushuka kwa umaarufu wa bwana Abe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728