02 Julai 2015

Majeshi ya Misri yaua wapiganaji wa IS

Shambulio la bomu katika peninsula ya Sinai
Wapiganaji wengi wa Kiislam wa kundi la Islamic State wameripotiwa kuuawa katika mapigano makali kati ya majeshi ya usalama ya Misri na
kikundi hicho katika peninsula ya Sinai, kaskazini mwa Misri. Mapigano yalidumu kwa saa kadha kuzunguka mji wa Sheikh Zuwaid, kwa serikali kupeleka ndege na helikopta za kivita.
Mbali na kuuawa kwa wapiganaji wa Islamic State, wanajeshi na raia ni miongoni mwa waliopoteza maisha.
Habari kutoka mjini Cairo, Majeshi maalum ya usalama ya Misri yalizingira jengo moja na kuwaua wafuasi tisa wa kikundi cha Muslim Brotherhood. Wizara ya mambo ya ndani imesema watu hao walishukiwa kupanga mfululizo wa mashambulio. Kikundi cha Muslim Brotherhood kimesema wafuasi wake tisa waliuawa kikatili na kimewataka wafuasi wake kufanya maasi dhidi ya Rais Abdel-Fattah el-Sisi.
Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa pia wakiendesha mashambulizi katika nchi za Syria na Iraq kwa lengo la kuzitawala nchi hizo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728