16 Julai 2015

Nyumba ya Chris Brown yavamiwa

Chris Brown
Nyumba ya nyota wa muziki Chris Brown kutoka Marekani imevamiwa na kupekuliwa na watu watatu waliofunika nyuso zao ambao walimfungia shangazi lake ndani chumba chake kulingana na
maafisa wa polisi.
Nyota huyo wa muziki wa R&B hakuwepo nyumbani kwake wakati wa wizi huo ambao ulifanyika alfajiri siku ya jumatano.
Maafisa wanasema kuwa washukiwa ambao walikuwa na bunduki waliondoka katika jumba hilo la Tarzana na fedha za kiasi kisichojulikana pamoja na vitu kadhaa vya kibinafsi.
Brown au wawakilishi wake bado hawajatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.
null
Chris Brown na Rihanna kabla ya wawili hao kukosana
Kulingana na ripoti,nyota huyo alikuwa ameenda kujivinjari katika kilabu moja wakati wa kisa hicho
Hii ni mara ya pili ya nyumba ya msanii huyo ambaye alikuwa mpenziwe nyota wa muziki wa Pop Rihanna kuvamiwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.
Mnamo mwezi Mei,aliwasili nyumbani na kumpata mwanamke mmoja aliyedaiwa kuvunja na kuingia kupika vyakula kadhaa na kuandika ukutani kwamba anampenda msanii huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728