28 Julai 2015

Uingereza ,Ufaransa kuwakabili wahamiaji

Wahamiaji wakiingia ndani ya magari ili kuvuka mipaka
Kampuni wa usafiri inayofanya safari zake kati ya Ufaransa na Uingereza ya Eurotunnel imesema maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakijaribu kuingia
nchini Uingereza kupitia usafiri huo.
Ripoti ya kampuni hiyo imebainisha kuwa idadi ya majaribio ya wahamiaji kutaka kuvuka mpaka kupitia usafiri aina hiyo ya usafiri imeongezeka mno,kwani wahamiaji hao watu hao wanajificha kwenye magari ya mizigo,kupanda vizuizi ilimradi tu waingine katika vyombo hivyo vya usafiri na kuvuka.
Katika mkutano wa Mawaziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa na Uingereza uliofanyika mjini London,mbinu za pamoja kuweza kudhibiti wahamiaji hao kuvuka zimejadiliwa na kuelezea hali kuwa ni tatizo kubwa kwa sasa.
Wahamiaji hao kutoka nchi za Sudani na Afghanstan waliopo bandari ya Calais nchini ufaransa ya Calais ndiyo waliobainika kutaka kuvuka kwenda nchini Uingereza kwa mfumo huo, wengi wa wahamiaji hao wanatoka nchini Sudan na Afghanstan.
Mwaziri hao wa mambo ya ndani wa Ufaransa na Uingereza wanasema wamebaliana tutafanya kazi pamoja kuwarejesha wahamiaji hawa ambao wengi wao wanatoka Afrika Magharibi,na kuwahakikishia watu kwamba safari za aina hii haziwi lango kuu la wahamiaji kuingia Uingereza.
Na tayari serikali ya Ufaransa imekwisha anza kuweza jitihada za ziada kama idadi zaidi ya askari,na uingereza itatoa kiasi cha paundi million saba kuimarisha ulinzi,japo kuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya Claude Moraes anasema haamini kama hatua ya kuwarejesha wahamiaji hao makwao kutasaidia kutatua tatizo hilo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728