12 Julai 2015

Waziri mkuu wa Serbia Vucic apigwa mawe

Waziri mkuu wa Serbia Vucic apigwa mawe
Waziri mkuu wa Serbia Aleksandar Vucic,amepigwa mawe na kufukuzwa na raia wa Bosnia katika hafla ya ukumbusho wa miaka 20 ya mauaji ya
halaiki ya watu katika mji wa Srebrenica
Waziri huyo alilazimika kutorokea maisha yake bada ya kutupiwa chupa mawe na matusi.
Mashamblizi hayo yalitokea bwana Vucic alipokuwa akiondoka kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa katika makaburi ya takriban wahanga 136 wa mauaji hayo.
null
Inaaminika kuwa waziri Vucic aligongwa na jiwe kichwani.
Inaaminika kuwa waziri Vucic aligongwa na jiwe kichwani.
Vikosi vya majeshi ya Bosnia Serb viliwaua wanaume 8000 waisilamu na wavulana wa Srebrenica baada ya kuvamia kambi ambayo ilistahili kulindwa na umoja wa mataifa.
Mauaji hayo yanadaiwa kuwa ndiyo yaliyoisababisha Yugoslavia kuvunjika.
null
Hii leo sherehe hizo zitakamilika kwa maziko ya waathiriwa136
Hii leo sherehe hizo zitakamilika kwa maziko ya waathiriwa136 ambao mabaki yao yalitambuliwa hivi majuzi kwa kutumia DNA.
Rais wa zamani wa marekani Bill Clinton ni mmoja wa wale wanaodhuruia maadhimisho hayo.
Awali waziri mkuu Vucic alikuwa ametoa risala za rambirambi japo aliepuka kukiri kuwa yalikuwa mauaji ya halaiki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728