07 Mei 2015

Barua Nzito Wema Kuna Kitu cha Kujifunza kwa‭ ‬Zari‭!

Barua Nzito Wema Kuna Kitu cha Kujifunza kwa‭ ‬Zari‭!
     KWAKO mtoto mzuri, Beutiful Onyinye, Wema Sepetu !'Madam'. Vipi uko poa? Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima namshukuru Mungu, hofu na mashaka ni kwako wewe uliye mbali na upeo wa maisha yangu.
    Kitambo kidogo hatujaonana, nimeona si mbaya kama nitakukumbuka kwa barua maana najua kutokana na majukumu yako na yangu kuwa mengi, wakati mwingine tunaweza tukafikisha hata miezi sita hatujaonana.
    Dhumuni la barua hii ni kutaka kukushauri kwamba unaweza kujifunza kitu kutoka kwa mpenzi wa sasa wa aliyekuwa mpenzi wako, Nasibu Abdul !'Diamond, Zarinah Hassan !'Zari!
    Naomba usinielewe vibaya. Sina nia ya kukupambanisha wala kutaka kukukejeli kwa namna yoyote. Kuna kitu kidogo tu cha kujifunza kutoka kwa binti huyo wa Kiganda.
    Achana na maneno yanayosemwa mtaani, kila mmoja ana upungufu wake lakini binadamu tunashauriwa kuiga yale mazuri kutoka kwa wenzetu.
    Iko hivi Wema, wewe na yeye mna nafasi moja nzuri katika jamii. Nyinyi ni maarufu. Mnapendwa na watu kupita maelezo. Mna ushawishi mkubwa sana katika jamii hivyo mnaweza kufanya jambo na likapata mafanikio makubwa sana.
    Umaarufu wenu ni biashara. Kwa nini uendelee kubaki chini wakati umezungukwa na fursa kibao? Umaarufu wako ni biashara kama utaamua kuwa !٪serious!& na kila hatua unayoipiga.
    Nikwambie ukweli bila unafiki, unapaswa kuiga jambo moja tu la msingi kutoka kwa Zari, kuwekeza na kuheshimu fedha.
    Mwenzako anaijua fedha. Anajua namna ya kuitafuta na namna ya kuiwekeza katika maeneo ambayo yatazidi kuzizalisha. Akili yake inawaza pesa na si starehe zisizokuwa na msingi.
    Mfano mdogo tu ni !٪idea!& kama ya All White Party aliyofanya Zari kule Uganda. Alifanikiwa, anaendelea kufanya na wiki iliyopita aliifanya pale Mlimani City jijini Dar na kupata mafanikio makubwa.
    Kwangu mimi kile ni kitu kikubwa sana ambacho kinaingiza fedha nyingi kwa wakati mmoja. Si vibaya kama utaiga vitu vya namna hiyo. Nisikufiche, nafasi ya umaarufu uliyonayo Kibongobongo, unaweza kufanya zaidi ya shoo ile kama utaamua na kupata watu wazuri wa kufanya nao kazi.
    Na unapofanya mambo makubwa kama hayo, lazima pia udhibiti matumizi yako. Starehe zipo lakini wakati mwingine unapaswa kuheshimu fedha. Yale mambo ya kwenda kuzimwaga ukumbini eti kuwa kama kina pedeshee nanilii!, si mazuri.
    Jeuri ya fedha ifanye kwa kufungua miradi mikubwa ambayo hata utakapozeeka utainjoi matunda yake. Kuigiza kuna mwisho, huwezi kuwa mwigizaji milele, kuna wakati utatakiwa kuwa msimamizi wa miradi yako tu binafsi na mkono uende kinywani kiulani tu.
    Usikubali kushikiwa akili na wapambe, unayoshauriwa na wapambe yachuje maana si yote yanakuwa na manufaa. Tumia kipaji na jina lako vizuri, una nyota ya kupendwa basi kupendwa huko kuwe na faida.
    Natambua una idea zako ambazo tayari umeanzisha kama kipindi chako cha In My Shoes, usiishie hapo fanya makubwa zaidi.
    Kwa leo acha niishie hapo. Ni matumaini umenielewa.

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
    KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

    TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

    POSITION DESRIPTION;

    Agricultural Technician

    Qualifications

    Diploma in agriculture

    Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

    apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728