Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu DunianI ( FIFA) Joseph Blatter ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) Jamal Malinzi kufuatia klabu ya Young Africans kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Katika salamu hizo za Blatter, amemuomba Rais wa TFF kufikisha salamu zake za pongezi kwa klabu ya Young Africans, wanachama, wapenzi wa mpira wa miguu kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mwakani katika michuano ya kimataifa barani Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Afisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, Blatter amesema anatambua mafanikio hayo ya kutwaa ubingwa, yametokana na na jitihada za uongozi, wachezaji, bechi la ufundi, madaktari, wanachama , washabiki na kila mmoja aliyeshiriki katika kufanikisha kutwaa Ubingwa huo.
Mpira wa miguu unapata mafanikio makubwa kwa kuvuka mipaka hadi kuwa kichochezi halisi cha maendeleo, unawasaidia wachezaji wa ngazi zote kuinua vipaji vyao na mbinu katika kuelekezwa na kubadilika wakati huo huo wakiwa wakiwa na nyoyo za ushirikiano.
Salamu kutoka kwa Blatter zinakuja wakati Afrika ikitangaza kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao wa FIFA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni