Bondia Kutoka Ufilipino Manny Pacquiao amefanyiwa upasuaji wa bega lake alilodai kuwa ndiyo iliyopelekea yeye kushindwa na Floyd Mayweather jumapili iliyopita.
Bondia huyo tayari anakabiliwa na kesi moja huko Nevada kwa kutosema ukweli kuhusiana na hali yake ya afya kabla ya pigano.
Hata hivyo daktari wake Neal ElAttrache, amesema kuwa amefurahia matokeo ya upasuaji huo licha ya ripoti kudokeza kuwa Pacquiao anahitaji muda wa mwaka mmoja kuuguza jeraha hilo.
Pacquiao mwenye umri wa miaka 36 alinyimwa dawa ya kupunguza maumivu kabla ya mechi alipokuwa akilalama kuteguka bega.
Hata hivyo imebainika kuwa kabla ya pigano hilo shirikisho la riadha na masumbwi ya kulipwa katika jimbo la Nevada lilipuzilia mbali ombi la shindano hiyo kwani haikuwa imearifiwa awali.
NAC inapendekeza kushtakiwa kwa bondia huyo mfilipino kwani hakusajili maumivu ya aina yeyote katika fomu maalum siku moja kabla ya pigano.
Kutokana na masaibu yake, mwanamasumbwi wa kulipwa Floyd Mayweather, 38,amejitokeza na kusema kuwa hana pingamizi ya kuchuana tena dhidi ya Pacquiao ila katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Awali mwanadondi huyo alikuwa amesema yuko tayari kuzichapa dhidi ya Muingereza Amir Khan miongoni mwa wanandondi wengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni