07 Mei 2015

Ray na Davina Kidogo Wazichape Ukumbini!

Ray na Davina Kidogo Wazichape Ukumbini!
  • Ray na Davina Kidogo Wazichape Ukumbini! 1
  • Ray na Davina Kidogo Wazichape Ukumbini! 2
Mastaa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Halima Yahaya ‘Davina’ nusura wazichape kavukavu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar baada ya Ray kudaiwa kumshika mwenzake huyo sehemu nyeti, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti la Risasi, ambacho kilikuwa shuhuda wa tukio hilo, Davina alikuwa amekaa na wasanii wengine pamoja na Mlezi wa Bongo Movies, mama Loraa wakipata vinywaji ndipo Ray alipofika na kuharibu shughuli.

“Wakati Davina anaendelea kupata kinywaji na mama Loraa, alitokea Ray akiwa tayari ‘ameshakula vyombo’ na kumshika Davina kalio kitendo kilishomkasirisha sana msanii huyo na kuanza kumcharukia Ray,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Davina alinyanyua glasi ya kinywaji chake, akammwagia Ray huku akimuuliza kwa nini alimshika makalio ndipo Ray naye alipopandisha hadi wakataka kukunjana.”
Baada ya vurugu hizo kuanza kushika kasi, alitokea mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wenzake ambao waliwasihi wawili hao waachane na mambo hayo.

Baada  ya kupata habari hiyo, gazeti hilo liliwatafuta wahusika ambapo lilianza na Davina.
“Jamani mi nafikiri nisizungumzie hilo tukio maana naona ni la aibu, si kitendo kizuri na kinaniumiza mno kwa maana ni udhalilishaji mno na kwa nini mtu akufanyie hivyo?,” alisema Davina. Simu ya Ray iliita bila kupokelewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728