07 Mei 2015

Lulu: Sina Jini Mauti

Lulu: Sina Jini Mauti
Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael `Lulu’ amekanusha uvumi kuwa matatizo yanayowatokea wanaume aliowahi kuwa nao yanatokana na yeye kuwa na Jini Mauti anayesababisha hali hiyo kutokea.

Akizungumza na gazeti la Amani juu ya madai ya wadau mbalimbali kuhusiana na matukio mengi yanayomtokea, staa huyu ambae ni mrembo, alisema maisha yake ya siku hizi ni ya kusali sana, hivyo anaamini kutokana na maombi yake, hali yake iko vizuri kutokana na Mungu kumpa anachokihitaji.
“Ninasali sana kwa sasa aisee, mara nyingi nafanya hivyo mara tatu kwa siku, ninao uwezo wa kukemea mapepo na yakaondoka, hayawezi kukaa mwilini mwangu,” alisema muigizaji huyo ambaye miaka michache iliyopita, aliondokewa na mpenzi wake, Steven Kanumba aliyeanguka na kufariki mbele yake.
Mtabiri mmoja maarufu jijini Dar es Salaam, Maalim Hassan Yahya Hussein, alisema tatizo kubwa linalomsumbua binti huyo ni jini mauti ambalo baada ya kumpenda, halitaki kuridhia uhusiano wake wa kimapenzi na binadamu.“Hapa nimshauri tu, achukue hatua ya matibabu haraka iwezekanavyo vinginevyo hali hiyo itaendelea, anatakiwa afanye kafara kwa kuchinja mnyama yoyote ili aondokane na matatizo haya,” alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728