Staa mrembo wa filamu, Husna Chobis amefunguka kwa kusema kuwa filamu alizoigiza za kiasili zimepata dili la kwenda kuigiza nchini Uingereza, baada ya kuchaguliwa kupitia sinema ya Gawa na Ndase alizoigiza na kumpatia umaarufu.
“Namshumkru Mwenyezimungu kwa kuonyesha kipaji changu uigizaji na hasa filamu za asili, najua wazi kama si filamu hizi isingekuwa rahisi kuchaguliwa na kuja hapa Uingereza kushiriki filamu ninayocheza sasa, filamu za asili zimenipa dili,”anasema Husna.
Msanii huyo yupo nchini uingereza pamoja wasanii wenzake wawili yaani Eshe Buheti na Yusuf Mlela zaidi ya mwezi mmoja wakirekodi filamu inayoshiriki raia wa Afrika ya Mashariki na wasanii kutoa Afrika Magharibi nchi za Naijeria na Ghana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni