Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud, amesema kuwa Somalia na Kenya zinafaa kuimarisha uhusiano wao dhidi ya ugaidi, baada ya wapiganaji wa kiislamu kushambulio chuo kimoja kikuu mjini Garrisa hapo jana Alhamisi.
Bwana Mohamoud ametaja mauaji hayo kama tendo la kinyama ambalo halina msingi katika dini ya kiislamu.
Ametoa rambirambi zake kwa serikali ya Kenya.
Kenya imetoa zawadi ya shilingi millioni 5 kwa mtu yeyote atakayeweza kumkamata Mohammed Kano ,mwalimu wa zamani ambaye anashukiwa kupanga mauaji hayo.
Kwa sasa anaidaiwa kuwa nchini Somalia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni