Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Wema Sepetu amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema kuwa hata yeye anampa pongezi mpenzi wake wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa jitihada alizozifanya mpaka kufikia hatua ya kumaliza nyumba yake iliyopo Madale jijini Dar.
Akizungumza na gazeti la Ijumaa, Wema alisema kuwa hata kama hawako pamoja lakini kama kuna kitu cha kumsifia kwa jambo zuri alilofanya hana sababu ya kukaa kimya na akinyamaza atakuwa mnafiki.
“Nikikaa kimya bila ya kumpongeza Chibu nitakuwa mnafiki, amefanya jambo zuri la kuigwa hivyo binafsi nampongeza kwa hapo alipofikia,” alisema Wema ambaye katika hatua za mwanzo za ujenzi huo alishiriki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni