Rais wa Palestina Mahmoud Abbas
amekataa kukubali mamilioni ya dola ambazo ni fedha za kodi ambazo
zilikuwa zimezuiliwa na Israeli.
Bwana Abbas alisema kuwa aliamua
kurudisha pesa hizo kwa sababu Israeli ilikuwa imekata kiasi fulani ili
kulipa kile ilichosema kuwa ni madeni kwa makampuni ya nchi yake.Bwana Abbas alisema kuwa pesa zilizokatwa ni kama thuluthi moja ya pesa zote ambazo Israeli imekuwa ikizuia.
Amesema kuwa iwapo Israeli itakosa kulipa fedha zote hizo atapeleka kesi katika mahakama ya haki ya kimataifa ICC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni