
Serikali ya Kenya imeitetea idara
yake ya usalama kufuatia shutma kwamba ilichelewa kukabiliana na
shambulio la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 150 waliuawa.
Shambulio hilo lilisitishwa baada wapiganaji wanne waliohusika kuuawa na maafisa wa polisi saa 15 baada ya kuvamia chuo hicho.
Lakini naibu wa rais William Ruto anasema kuwa kundi la kwanza la
polisi liliwasili katika chuo hicho saa moja baada ya shambulizi.

Amelipongeza
jeshi la Kenya KDF kwa kile alichokitaja kua hatua za haraka.Lakini
vyombo vya habari vimekuwa vikisema kuwa vikosi maalum vilivyowaua
wapiganaji hao vilichelewa kufika katika eneo hilo kutokana na mfumo wa
usafiri waliotumia.

Pia kuna madai kwamba maafisa wa polisi walifeli kuchukua hatua za
dharura baada ya kupewa habari kwamba mmoja ya wauaji ambaye sasa
ametambuliwa kama Abdirahim Abdullahi ni wakili na mwana wa chifu mmoja
katika eneo la kazkazini mashariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni