Staa mrembo wa Bongo Movies, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema kuwa
migogoro yote inayomtokea aliyewahi kuwa mwandani wake, Emmanuel
Elibariki ‘Nay’ ni kutokana na laana ya kumsambazia picha zake za utupu.
Akipiga stori na paparazi wa GPL, Bozi alisema tatizo kubwa
lililomkuta Nay kwa mpenzi wake Siwema kumfumania na njemba ni malipo ya
kupuuza penzi lake na dhambi kubwa aliyomtendea ya kusambaza picha zake
za utupu alizomtumia wakati walipokuwa kwenye uhusiano.
“Nilimpenda mno Nay lakini fadhila ya penzi langu akaona
anidhalilishe kwa kuanika picha zangu za utupu kwenye mitandao ya
kijamii, jambo linalonisononesha mpaka kesho, naamini yaliyomtokea ni
laana yangu anayotembea nayo kwani bado sijamsamehe kwa kitendo kile cha
ajabu alichonifanyia,” alisema Bozi.
06 Aprili 2015
Bozi: Nay wa Mitego Ana Laana Yangu
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni