Wakristo nchini Kenya wametumia
maadshimisho ya misa za sikukuu ya pasaka kote nchini humo kuwaomboleza
waathirika wa mauaji ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa.
Makanisa
mengi nchini humo yaliomba ulinzi wa askari wenye silaha kuwalinda
wakati wa ibada .Ibada hizo zilikuwa maalumu kuwaombea marehemu wapatao
mia moja na arobaini na nane waliouawa na kundi la wanamgambo wa Al
Shabaab ambao waliwalenga wakristo zaidi katika shambulio hilo.Wengi wa wanafunzi mia moja na arobaini na nane waliouawa walikuwa ni wakristo waliochambuliwa na magaidi wenye silaha wa kundi la Al shabaab.
Katika siku ya kwanza ya maombolezo ya kitaifa makanisa mengi yalilindwa na walinzi wenye silaha.
Askofu wa Kanisa kuu la Garissa Joseph Alessandro amesema mashambulizi yametengeneza alama kwa watu.
"Hali ya wasi wasi na uoga imekuwa ya kila siku, kwa sababu haya mashambulizi yamekuja kwa kushtukiza, hukuwa umejiandaa na hivyo hali hii inafanya kuwa katika hali ya wasi wasi muda wote."
Mmoja kati ya waumini waliohudhuria ibada hiyo anasema amepata faraja ndani ya kanisa.
"Hakuna mahali popote ambapo ni salama, lakini hapa kanisani unaweza kuja na ukampokea Mungu ambaye anakuwezesha kujifariji wewe mwenyewe."
Wakati huo huo,vilio na majozi viliendelea kwa ndugu waliokwenda kutambua miili ya wapendwa wao waliouawa katika shambulio hilo la kigaidi.
Baadhi ya waliofika kutambua miiili ya ndugu zao wamesema zoezi la kutambua miiili limekuwa gumu.
"Imetuchukua takribani dakika 20 miili imeharibika ipo nje, imepoteza maumbo yake hivyo inachukua muda mrefu kutambua ndugu zetu."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni