Staa mkongwe wa Bongo Movies, Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’ kwa mara ya kwanza ataibuka kama mwanamke katika filamu inayokwenda kwa jina la ‘ Nimekubali kuolewa’ inayotarajiwa kutoka Mei 21 mwaka huu baada ya kucheleweshwa kutoka na bodi ya filamu nchini ambayo ilikuwa na wasiwasi nayo katika baadhi ya vipengele.
Akizungumza na gazeti la Sani, Dokta Cheni alisema kwamba filamu hiyo ni nzuri na imefanyika katika ubora wa hali ya juu.
Aidha, alikiri kusimamishwa na bodi ya filamu na kusema kwambaalijitahidi kuwaelewesha baadhi ya vipengele ambavyo viliikwaza bodi, anashukuru walimuelewa.
Wakili walichoza filamu hiyo ni pamoja na Dokta Cheni, Steve yanga (sasa hivi Azamu) Gabo Zigamba, Mzee Mapendo, Mzee Nyau na wengine wengi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni