Meya wa mji wa Boston Martin Walsh amesema kuwa ana matumaini kuwa hukumu ya kifo aliyopewa mshambuliaji kwenye mbio za Boston Marathon itawapa nafuu wale wote walioathiriwa na shambulizi hilo.
Iliwachukua majaji saa 14 kuamua ikiwa Dzhokhar Tsarnaev atauawa kwa kudungwa sindano ya sumu badala ya kupewa kifungo cha maisha.
Waathiriwa kadha walielezea kuridhika kwao wakisema kuwa uamuzi huo utawawezesha kuendela na maisha yao.
Wengi wanahofu kuwa ikiwa rufaa itakatwa, itawaongezea machungu zaidi moyoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni