Maafisa wakuu katika idara ya ulinzi ya Marekani wamekiri kuwa chembechembehai za ugonjwa hatari wa Kimeta zilitumwa kimakosa kwa kambi 9 za
kijeshi nchini Marekani na moja nchini Korea Kusini.
Kulingana na makao makuu ya ulinzi nchini Marekani sampuli za chembechembehai za Kimeta zilidhaniwa kuwa zimekufa na hivyo zikatumwa kutumia njia ya usafirishaji mizigo ya umma kimakosa.
Chembechembe hizo za kimeta zilikuwa zimenuiwa kutumika katika mazoezi ya shambulizi la zana za kibaiolojia zakijeshi katika kambi za mazoezi.
Wandani wa maswala ya zana za kibayolojia wanasema kuwa kungetokea maafa makubwa iwapo chembechembe hizo za kimeta zingeachiliwa nje ya maabara maalum ya kibayolojia.
Maafisa wa serikali ya Marekani walioko Korea Kusini wameripoti kuwa takriban watu 22 waliogusana na zana hiyo katika kambi ya kijeshi ya Osnan wanachunguzwa.
Hadi sasa hakuna kati yao aliyeonesha dalili za maambukizi ya ugonjwa huo hatari.
Wakati ukweli ulipobainika mahabara na vituo vya kijeshi vilifungwa.
Kimeta ni hatari ikinuswa au ikiliwa.
Ni silaha inayoweza kutumiwa wakati wa vita vya kemikali.
Makao makuu ya kijeshi ya Pentagon yanasema kuwa haijulikani ni watu wangapi wanaokabiliwa na hatari hiyo nchini Marekani.
Hadi uchunguzi ukamilike, hakuna bacteria zozote za kimeta zinaweza kusafirishwa kutoka Marekani.
Kambi za kijeshi zilizoathirika ni Texas, Maryland, Wisconsin, Delaware, New Jersey, Tennessee, New York, California na Virginia.
Kufikia sasa watu wanne pekee wanachunguzwa nchini Marekani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni