Kiongozi wa harakati za Shia wa Hezbollah Hassan Nasrallah amesema dunia inakabiliwa na hatari kubwa kuwahi kutokea katika historia kutokana na
makundi ya kigaidi ya Islamic State na Al-Qaeda yanayopigana nchini Syria .
Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada Waziri wa ulinzi wa Marekani kuyashutumu majeshi ya Iraq kwa kukosa ari ya kupambana na wapiganaji wa Islamic State.
Akihutubia maefu ya wafuasi wake kwa njia ya video kiongozi huyo wa Hezbollah Sheikh Nasrallah amekiri kwa mara ya kwanza kuwa Hezbollah imekuwa ikipigana muda wote maeneo ya jirani na Syria kumsaida Rais wa Syria Bashar al-Assad.
"Kila mtu anapaswa kuona kuwa yupo kwenye hatari,na wala hii si hatari kwa wale wanaolengwa na wapiganaji hao tu, ama Lebanon,Serikali ya Iraq na makundi ya Yemen, hapa hii ni hatari kwa kila mmoja. Hakuna atakayezika kichwa chake ardhini kuepuka mapigano hayo, ndiyo tunapigana kwaajili ya ndugu zetu wa Syria,jeshi na wakazi wa Syria katika miji ya Aleppo,Homs ,Deir Ezzor ,Qalamoun,Hasakeh na Idlib".anasema Shekh Nasrallah
Naye Waziri wa ulinzi wa Marekani,ameyashutumu majeshi ya Iraq kwa kukosa morali ya kupambana na wapiganaji wa Islamic State.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida ya maoni hayo ya lawama,Ash Carter amesema kwamba majeshi yao yana idadi kubwa ya askari katika mji wa Ramadi,lakini yalitimuliwa mjini humo baada ya kukabiliana na Islamic State.
Naye Waziri mkuu wai Iraq Haider al-Abadi ameambia BBC kuwa vikosi vyake vitaukomboa mji wa Ramadi kutoka kwa wanamgambo wa islamic state siku chache zinazokuja.
Mapema msemaji wa jeshi la Iraq alipinga shutuma kutoka kwa waziri wa ulinzi nchini marekani -Ash Carter -kuwa jeshi la iraq halima motisha ya kupigana.
Bwana Ash amesema kuwa marekani itaenndelea kuwapa mafunzo na kuwapa salaha wanajeshi wa Iraq lakini aliongeza kuwa wataishinda tu ISIS ikiwa watajibu kwa kupigana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni