Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu amesema alipokuwa akihojiwa na Sebo mtangazaji wa EFM, kwenye kipengele kiitwacho Kabali ambapo wema aliambiwa ajibu maswali kadhaa kama ndiyo au hapana na badaye kupewa nafasi ya kifafnua.
Wame aliulizwa kama bado anampenda Diamond, na kama Zari ni tishio kwake kwa upande wa fasheni ambapo yote hayo Wema alijibu hapana na kijibu ndiyo alipoulizwa kama yeye ni Team Kiba.
Akifafanua kuhusu kuhusu kutompenda tena Diamond Wema alisema kuwa kila kimkumbuka Diamond anamkumbuka kwa mengi mabaya .
“Hapana simpendi [Diamond], yalishaisha hayo, nilishampendega, niliwahi kumpenda sana, lakini hamna tena, yaani hata sishtuki,” Wema alisema.
“Nikimkumbuka Diamond most of the things ambavyo ninavikumbuka sio vitu vizuri na ndio maana hata sasa hivi imekuwa hivyo. Vizuri vilikuwepo lakini mtu anaweza akafanya vizuri akaja kufanya kimoja tu kibaya na akaharibu vyote tisa,” aliongeza.
Kwa upande wa Zari ambaye ni mpenzi wa sasa wa Diamond, Wema alieleza kutoitishika na mwanadada huyo kwenye tasnia ya fasheni.
“[Zari] hanitishi kwasababu yeye ana taste yake, mimi nina taste yangu, yeye ni Zari mimi ni Wema,” amesema muigizaji huyo. “I got my own, I like to play along with anything and she got her own.”-Wema alisema.
Zaidi alizungumzia gari aina ya BMW alilipewa mwaka jana na meneja wake Martin Kadinda kwenye sherehe za siku yake ya kuzaliwa, Wema alisema kuwa Martin alipita sehemu nyingi na kufanya donation walifanya dada zake walioko marekenai na yeye hajui ilikuwaje hadi gari likapatikana pia wema amesema kuwa kwasasa hawezi ku-date na msanii yoyote hapa Bongo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni