Maelfu ya Wakatoliki wanahudhuria sherehe mjini Nyeri, Kenya, ya kum'bariki mtawa wa kale kutoka Italia.
Irene Stefani aliwasaidia majeruhi wa Afrika Mashariki, wakati wa vita vya kwanza vya dunia, kabla ya kufariki kutokana na tauni mwaka 1930.
Mji wa Nyeri umejaa maelfu ya watu na wengi walikesha hapo jana.
Mabaki ya mtawa huyo yatasafirishwa hadi kanisa kuu la Nyeri siku ya jumapili.
Wakatoliki wanaamini kuwa alionyesha miujiza baada ya kufa, katika mwaka wa 1989, pale watu waliokuwa wakikimbia vita vya Msumbiji, walipoomba kwa jina lake.
Wanasema maji yalitiririka kutoka mbele ya kanisa, na kunusuru maisha ya waliokuwa na kiu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni