26 Mei 2015

Gari za kijeshi zatumika kubeba maharusi

Wakala wa harusi wanadai magari ya kifahari (limo) hayana shamrashamra
Wakala wa maandalizi ya Harusi mjini Moscow wamewakodishia magari ya kivita( Deraya) maharusi wapya ili
yawasindikize kwenda kwenye sherehe yao badala ya kukodi gari ya kifahari aina ya limo kwa madai kuwa hayaleti shamrashamra katika sherehe.
Wakati magari hayo ya Deraya ni kawaida kuonekana katika mitaa ya Moscow kwa ajili ya gwaride za kijeshi, kwani hukodiwa katika safari za migahawa au ofisi au wakati wa kampeni kwa thamani ya dola 2,000 au Euro1,300.
Meneja wa wakala hao ameiambia Televisheni ya Urusi, NTV kuwa kila kitu hutegemea usajili,Kama wewe usajili wako ni kuendesha gari kando ya Barabara ya Moscow au katikati basi gharama zinatofautiana;kodi ya gari ya Deraya itakuwa ghali zaidi, na kama unataka kutumia pesa kidogo basi inabidi kuepuka kutumia barabara za katikati ya jiji kabisa na kutoka nje kidogo. Afisa wa polisi aliiambia Redio ya Ekho Moskvy kwamba kazi ya magari ya Deraya ni kuchukua vifaa vikubwa na kwa hiyo kuna haja ya ruhusa maalum kutoka mamlaka husika na uratibu wa Polisi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728