Mwanajeshi mmoja nchini Tunisia amempigwa risasi na kuuawa baada ya kuwaua wenzake 7 .
Askari wengine 10 walijeruhiwa mmoja wao akiwa hali mahututi katika shambulizi lililotokea katika hafla ya kupeperusha bendera katika kambi ya kijeshi ya Bouchoucha.
Kwa mujibu wa msemaji wa idara ya ulinzi Belhassen Oueslati askari huyo alikuwa na matatizo ya kifamilia na kiakili.
Wakati wa tukio afisa huyo alikuwa amekatazwa kubeba silaha yeyote.
Duru zinasema kuwa askari huyo alimiminiwa risasi na kuuawa pia na wenzake, ili kumzima asiendelee kutekeleza maafa hayo kisha utulivu ukarejelewa.
Wakuu wamekanusha kuwa kisa hicho kilichofanyika katika kambi moja ya kijeshi mjini Tunis, sio ya kigaidi.
Lakini kilisababisha taharuki kubwa mjini humo, ambapo mnamo mwezi Machi, wapiganaji wa kiislamu waliokuwa na silaha waliwauwa zaidi ya watu 20, wengi wao watalii, baada ya kuvamia makavadhi ya Bardo mjini Tunis.
Bwana Ouselati alisema kuwa afisa huyo alimshambulia afisa mmoja kwa kisu kabla ya kumpokonya bunduki na kuitumia kuwashambulia maafisa wengine.
Aliongezea kusema kuwa ''ninahakika kuwa hilo lilikuwa tukio la kipekee wala sio la kigaidi''
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni