25 Mei 2015

B.Faso:mwili wa Thomas Sankara kufukuliwa

Mwili wa Thomas Sankara kufukuliwa leo Burkina Faso
Ripoti za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unakisiwa kuwa wa raisi wa
zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake.
Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku iwapo mabaki hayo ni yake.
Bwana Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987.
Sankara alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983.
Sankara alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa wa nchi hiyo Ouagadougou.
Mjane wa Sankara, Mariam
Madaktari wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa watachukua chembechembe za mwili huo na kuipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara.
Miili mingine 12 ya wafuasi wake waliouawa pamoja naye pia itafukuliwa.
Mabaki hayo ya Sankara yamezikwa katika makaburi ya Dagnoen katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Familia yake inashuku kuwa huenda mwili huo sio wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728