Ishara za mapema kutoka kwa kura ya maoni kuhusu uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini Ireland zinaonyesha kuwa wanaounga mkono ndoa hizo wanaelekea kupata ushindi mkubwa.
Kura zinaendelea kuhesabiwa na matokeo rasmi yanatarijiwa kutangazwa baadaye leo.
Lakini mawaziri wa serikali ambao wanaunga mkono mabadiliko hayo ya kikatiba,wameielezea siku ya leo kama ya kihistoria huku wengi waliopinga kura hiyo wakiwapongeza waliounga mkono sheria hiyo ya ndoa za jinsia moja.
Iwapo mabadiliko hayo yataidhinishwa,Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuruhusu ndoa za jinsia moja kupitia wingi wa kura.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni