Kocha wa klabu ya Liverpool, England Brendan Rodgers amesema yupo tayari kuondoka klabuni hapo, pale tu wamiliki wa timu hiyo watakapomtaka kufanya hivyo.
Liverpool imejikuta ikiaibishwa kwa kukubali kichapo cha bao 6-1 kutoka kwa Stoke City katika mchezo wa kufunga pazia la ligi kuu ya England, lakini pia mchezo huo ndio ulikuwa wa mwisho kwa nahodha Steven Gerrard. "mengi yamepita mwaka huu ambayo yameifanya kazi kuwa ngumu. Msimu uliopita wakati mambo yalipoenda vizuri, tuliungwa mkono na kila mtu, lakini kiwango cha sasa hakiwezi saidia na kiukweli naelewa hilo" alisema Rodgers.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni