Waziri mkuu nchini Ireland Enda Kenny amesema kuwa Ireland ni nchi ndogo iliyo na ujumbe mkubwa baada ya kupiga kura kwa wingi kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Mabadiliko hayo ya katiba yaliungwa mkono na zaidi ya asilimia 60 ya wapiga kura kwenye kura ya maoni ya siku ya Jumamosi.
Kanisa katoliki lilifanya kampeni ya kupinga kura hiyo.
Askofu mkuu wa mji wa Dublin Diarmuid Martin alikubali kushindwa na kusema kuwa matokeo hayo ni ishara ya mabadiliko ya kijamii nchini Ireland.
Wale waliokuwa wakiunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja waliitaja siku ya jana kuwa ya kihistoria nchini Ireland.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni