Staa wa Bongo Movie ambaye kwa sasa anaishi ughaibuni, Lucy komba ameamua kuelezea tuhuma zinazomkabili za kua na uhusiano wa kimapenzi na Hamad Ndikumana, aliekua mme wa msanii mwenzake Irene Uwoya.Akizungumza na
gazeti la sani Lucy ameelezea kwamba hakuna jambo lolote linalowakutanisha na Hamad zaidi ya filamu iitwayo "Kwanini nisimuoe" inayohusisha watu wawili tu.
Lucy alisema walipokua wanarekodi filamu hiyo ndio uvumi mwingi ulianzishwa. Ingawa mashabiki wengi walipinga kuwa haiwezekani filamu nzima ikahusisha watu wawili tu na kwamba hao wawili wanauhusiano lakini Lucy amesema kwamba filamu hiyo ikitoka itatoa majibu yote na amewasisitiza mashabiki wainunue filamu hiyo ya "kwanini nisimuowe".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni