Binadamu tuliumbwa kuishi katika misingi ya ubinadamu na sio unyama kama waishivyo wanyama wa porini leo naomba kusema kutoka moyoni mwangu.. Najua kabisa nina wazazi wangu ndugu zangu na
zaidi sana Mungu wangu ila kuna watu mpaka nakufa kamwe sintowasahau katika kuta za moyo wangu katika kipindi changu kigumu nilichopitia mlikuwa nembo namboni kubwa katika kuokoa maisha yangu...
Napenda kusema kuwa hata kwa haya yote tunayopitia bado ni madogo sana kuficha thamani yenu mliyoijenga juu yangu.
Nakumbuka sana mlipojitoa kwa ajili yangu mlipojinyima kwa ajili yangu mlipopigana kwa ajili yangu,mlivyofedheheka kwa ajili yangu yote hayo nayakumbuka na namshukuruu mungu kwani naona kabisa mliletwa duniani kwa sababu nyingi na moja ya sababu ilikuwa kuniokoa katika kipindi kigumu katika maisha yangu.
Leo hii tarehe 25.5.2015 napenda kusema kwa umma na zaidi kwa Mungu wangu kuwa nawathamini nawapenda na nashukuruuu sana kwa yote mliyofanya juu yangu.
Nawaombea kwa Mungu muendelee na moyo huo huo kwani naamini kuna wengi bado wanawategemea ili kukomboa maisha yao kwa wakati aliyopanga mungu
Hata kitabu cha dini kilisema kuwa "huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona" najua siku moja tutaishi kama zamani.. Ahsanteni
Hata kitabu cha dini kilisema kuwa "huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona" najua siku moja tutaishi kama zamani.. Ahsanteni
Kajala ameandika hayo kwenye ukursa wake kwenye mtandao picha wa Instagram mara baada ya kuweka picha hizo hapo juu ya Wema Sepetu na ya Petitman.
Michango ya wengi kwenye andiko hili, wamewataka Wema na Kajala muda umefika sasa wayamalize.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni