Waziri mkuu nchini Iraq Haider al-Abadi, anasema hawezi kuruhusu mji wa Ramadi kuingia mikononi mwa wanamgambo wa
islamic state ambao kwa sasa wanadhibiti sehemu kubwa ya mji huo ulio mji mkuu wa mkoa wa Anbar.
Serikali ya Iraq ilitangaza vita mjini humo.
Licha ya hilo bado majengo makuu ya serikali yamesalia mikononi mwa islamic state
Wapiganaji wa kundi la Islamic state walivunja vizuizi vya wanajeshi wa serikali kwa kutumia mashambulizi ya magari ya kujitoa mhanga siku ya ijumaa ambapo walidhibiti majengo muhimu na kuharibu makao makuu ya polisi.
Ndege za jeshi la Marekani zimeshambulia makao makuu ya islamic state karibu na mji wa Ramadi na makamu wa rais wa marekani Joe Biden ameahidi silaha nzito kwa jeshi la Iraq ilikukabiliana na wapiganaji hao.
Takriban milipuko 6 ya kujitolea mhanga ilitikisa mji huo kabla ya wapiganaji hao kuteka makao makuu ya serikali.
Takriban maafisa 50 wa usalama wanaamika kutekwa.
Maelfu ya wenyeji wa Ramadi wameanza kutoroka mji huo.
IS na majeshi ya Iraq yamekuwa yakikabiliana kwa muda mrefu kungangania udhibiti wa mkoa la Anbar.
Shambulizi hili la hivi punde linawadia siku moja tu tangu IS ichapishe sauti ya ya kiongozi wao Abu Bakr al-Baghdadi, ambaye alikuwa katangazwa kuwa alijeruhiwa vibaya mwezi machi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni