Frank (Mohamedi mwikongi)
Jina lake halisi ni Mohamedi Mwikongi ingawa wadau wengi wa bongo movies wanamfahamu kama “Frank”, ni mmoja wa waigizaji wakongwe sana ndani ya tasnia ya filamu nchini. Pamoja na kuwa na mwili uliojengeka vizuri kimazoezi pia Frank ni mwigizaji mwenye mvuto wa aina yake na ameweza kushiriki katika filamu nyingi sana hapa nchini. Anajulikana na mashabiki wake kama mwigizaji mstaarabu na mpole na mara nyingi kama mtu mwenye busara na maamuzi ya hekima.
Images
Movies
Early life
Frank alizaliwa jijini Dar es salaam tarehe kumi na nane( 18) mwezi wan ne (4) mwaka 1979 (18/4/1979) katka hospitali ya ocean road. Alipoanza kukua alihamia Mkoani Iringa ambako alipata Elimu yake yam sing katika shule ya msingi Wiloseli kabla ya kuhamia shule ya msingi Mapambano jiji Dar es salaam ambako alimaliza elimu yake ya msingi. Baada ya hapo alijiunga ma shule ya sekondari ya Highlands ilyopo wilayani iringa ambako alisoma na kuweza kuhitimu masomo yake ya O’level. Baadaye alijiunga na shuke ya sekondari Jitegemee kwa elimu ya kidato cha tano na sita na mwishowe kumaliza safari ya elimu katika Chuo cha kodi (ITA) cha TRA jijini Dar es salaam
Career
Mohamedi Mwikongi (Frank) alianza Rasmi kuigiza mnamo mwaka 1999 chini ya kikundi cha Fukuto arts group kilichokuwa kikirusha maigizo yake kwenye kituo cha ITV kabla ya kujiunga na kikundi cha Kaole sanaa group ambako aliweza kupata umaarufu mkubwa na kujenga jina lake la frank kwenye igizo la Tufani.
Baada ya hapo alianza kuigiza kwenye filamu mbalimbali na baadhi ya filamu zilizompa umaaarufu ni pamoja na Dangerous Desire, Sikitiko langu, behind the scenes na nyingine nyingi
Akiwa katika mapumziko Mohamedi anapenda zaidi kufanya mazoezi na kumpumzika
Contact Frank (Mohamedi mwikongi)
emwikongi@yahoo.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni