Kuwa na uzito mkubwa katika umri mdogo kunaweza kusababisha ugonjwa wa saratani ya utumbo hapo baadae
Watafiti walikuwa wakiwafuatilia wanaume takriban 240,000, Raia wa Sweden kwa miaka 35.
Uchambuzi uliochapishwa kwenye jarida moja, unaonyesha kuwa vijana wadogo walikuwa hatarini mara mbili zaidi kupata maradhi ya Saratani ya utumbo, takwimu zilikuwa juu zaidi kwa vijana wadogo wenye uzito mkubwa .
Shirika la kimataifa la utafiti wa Saratani limesema uhusiano kati ya uzito mkubwa na saratani una “nguvu”.
Saratani ya utumbo ni aina ya saratani ya tatu ambayo huwakumba walio wengi duniani, ikiripotiwa kugunduliwa kwa wagonjwa milioni 1.4 kila mwaka.
Ulaji wa Nyama nyekundu na matumizi ya Mafuta kupita kiasi husababisha uzito mkubwa.
Waliojitolea kwenye utafiti huo walikuwa na umri wa kati ya miaka 16 na 20 kwa kuanzia.Wengi wao walikuwa na uzito wa kawaida,
Rachel Thomson ni mtafiti kutoka Shirika la kimataifa la utafiti wa Saratani,amesema kuwa uzito wa kupita kiasi unaweza kusababisha Kansa ya utumbo
“Matokeo haya yanaonyesha kuwa Kansa ya utumbo inaweza kusababishwa na tabia na mtindo wa maisha yetu ya kila siku” alieleza Rachel
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni