28 Mei 2015

Nitabaki Real Madrid: Bale

Kiungo cha klabu ya Real Madrid Gareth Bale amesema atasalia katika timu hiyo.
Kiungo wa Real Madrid Gareth Bale ameelezea matarajio yake ya kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo msimu ujao, japokuwa kumekuwepo na tuhuma nyingi kutoka kwa mashabiki wa Madrid na baadhi ya
vyombo vya habari nchini Hispania kutoridhishwa na kiwango cha mwanandinga huyo ikilinganishwa na pesa zilizotumika kumnunua.
Bale ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter huku timu hiyo ikitangaza kuachana na kocha wake Carlo Ancelotti. "nitajituma katika kipindi hiki ambacho msimu umeisha na kutazama mbele juu ya kurejea tena kwenye msimu ujao nikiwa na nguvu pamoja na Real Madrid" aliandika Bale. Mchezaji huyo alijiunga na miamba hiyo ya soka nchini Hispania mwaka 2013 akitokea Tottenham na amekuwa akihusishwa kurejea tena katika ligi ya England.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728