Mahakama nchini Kenya imeamuru hospitali maarufu kulipa faini ya dola zaidi ya elfu 48 kwa kushindwa kuzuia uzazi .
Jaji alibaini kuwa mmoja wa wahudumu wa hospitali ya Aghakhan alizembea katika kupachika mwilini dawa ya kuzuia utungwaji wa mimba iliyochaguliwa na mwanamke kwenye mkono wake, licha ya kwamba mwanamke huyo alifanyiwa upasuaji mdogo kwa ajili ya kuzuia uzazi. Mwandishi wetu Anne Soy anarifu zaidi kuhusu uamuzi huo wa mahakama usio wa kawaida.
Muathirika aliimbia mahakama kuwa yeye na mumewe walikuwa tayari na watoto wawili na kwamba hawakutaka kupata mtoto mwingine . Kwa hiyo kutokana na ushauri wa hospitali mama huyo alipachikiwa dawa ya kuzuia uzazi ambayo ingelimzuia kupata ujauzito kwa miaka mitatu . Lakini mwaka mmoja baadae aligundua kuwa alikuwa mjamzito .
Ameiambia mahakama kwamba mimba ambayo hakuipanga ilimsababishia maumivu ya mfadhaiko mkubwa , msongo wa mawazo , matatizo ya kifedha na matatizo ya unyumba. Jaji alisema kuwa mshitakiwa ambae ni Hospitali ya Aga Khan , iliwasilisha nyaraka , lakini haikuwepo mahakamani wakati wa kesi hiyo .
Kesi iliendelea na hatimae jaji aliamua kuwa mhudumu wa hospitali alizembea kazini . Aliamuru mama aliyeshitaki hospitali ya Agakhan alipwe fidia ya dola elfu tano kwa hasara iliyosababishwa na apewe malipo ya dola elfu 43,000 za gharama ya maisha mtoto tangu kuzaliwa hadi atakapotimiza miaka 18.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni